Dodoma FM

Wakazi wa Asanje wamtaka mwenyekiti wa kijiji hicho ajiuzuru

18 May 2022, 2:49 pm

Na; Selemani Kodima.

Wananchi wa kijiji cha Asanje Wilayani Bahi  wamemtaka mwenyekiti wa Kijiji cha Asanje  Juma Dobogo kuachia nafasi yake kutokana kushindwa kuwatumikia na kusimamia Miradi ya kijiji .

Wakizungumza kwa Nyakati Tofauti katika Mkutano wa Kijiji wananachi hao wamelazimika kufikia hatua hiyo kutokana na kijiji hicho kuwa nyuma katika maendeleo licha ya uwepo wa mgodi wa  mawe ya chuma .

.

Baadhi ya wananchi hao wamesema wanashindwa kuona umuhimu wa kuwepo kwa Uongozi hao kutokana na kushindwa kutumiza wajibu wao ikiwa ni pamoja na kuhakikisha wanafatilia asilimia za kijiji zinazotakana na Mgodi wa mawe ya chuma.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa kijiji cha Asanje Juma Dobogo amesema tangu ameingia madaraka mwaka 2014  mpaka sasa  amekuwa akifutilia baadhi ya hatua ili kujua haki yao ya asilimia za kijiji zinazotkana na mgodi wa mawe ya chuma.

Akizungumzia hatua ya kutakiwa kuachia ngazi ,Mwenyekiti huyo amesema maamuzi ya wananchi kudai haki ni ya masingi kutokana na changamoto zilizopo kijiji hapo

Kutokana na hali hiyo, Mkuu wa wilaya ya Bahi Mwanahamisi Munkunda akizungumza nasi kwa Njia ya Simu amesema kitendo cha wananchi hao kushinikiza uongozi wa kijiji kufatilia mapato sio jukumu la uongozi huo bali ni halmashauri ya wilaya ambao wanawajibu wa ukusanyaji wa mapato.

Licha ya hayo kijiji cha Asanje ni miongoni mwa Vijiji venye changamoto kubwa hususani Barabaraba,maji,Nyumba ya mtendaji wa kijiji,Vyumba vya madarasa  na nishati ya umeme hali ambayo ni tofauti na kiasi cha mapato yanayokusanywa katika mgodi wa mawe ya chuma