Dodoma FM

Bunifu 26 kati ya 200 zafanikiwa kuwa bidhaa na kutumika

18 May 2022, 3:21 pm

Na;Yussuph Hassan.

Imeelezwa kuwa bunifu 26 kati ya 200 zilizoendelezwa na Tume ya Sayansi na Teknolojia Tanzania (COSTECH) zimefanikiwa kuwa bidhaa na kutumika katika sekta mbalimbali ikiwemo kilimo maji na nishati.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof Adolf Mkenda wakati akizungumzia mafanikio yaliopatikana katika wiki ya maonesho ya ubunifu yanayoendelea Jijini Dodoma.

Mkenda amesema kuwa bunifu hizo zimekuwa na msaada mkubwa katika sekta mbalimbali Nchini.

.

Naye Naibu Waziri wa Wizara hiyo Omary Kipanga amesema kuwa bunifu 200 zilizosalia zinaendelea katika hatua mbalimbali.

.

Maonesho ya kitaifa ya wiki ya Ubunifu yameandaliwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolijia yameanza May 16 kumalizika Ijumaa ya tarehe 20, 2022.