Dodoma FM

Maeneo ya kilimo cha umwagiliaji yatakiwa kuainishwa.

17 May 2022, 11:24 am

Na; Mindi Joseph.

Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe ameitaka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji kuainisha maeneo yanayofaa kwa umwagiliaji ambayo ni hekari milioni 29 .

Akizungumza katika uzindua Bodi ya Wakurugenzi jijini Dodoma Waziri Bashe ameitaka bodi hiyo kuziweka hekari hizo katika mfumo wa kidigitali ili wizara ya Kilimo iuwasilishe mchoro huo katika Wizara ya Ardhi.

Ameongeza kuwa shauku kubwa ya wananchi ya kutaka kuyaona mafanikio ya kilimo cha umwagiliaji, hivyo ni jukumu la Bodi hiyo kusimamia miradi kikamilifu na kuhakikisha inakuwa na tija.

.

Kwaupande wake Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Bw. Raymond Mndolwa ameahidi kuisimamia Taasisi anayoiongoza kwa weledi kufikia matarajio ya wananchi hususani katika Kilimo cha Umwagiliaji.

.

Akizungumza kwa niaba ya Bodi, Mwenyekiti wa Bodi ya Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Prof. Henry Mahoo amewataka Wajumbe wa Bodi na Menejimenti ya Tume ya Taifa ya Umwagiliaji kufanya kazi kwa kujituma ili kufikia malengo yaliyowekwa na serikali.

.