Dodoma FM

Asilimia kumi ya Watu duniani wanaishi na magonjwa sugu ya figo

17 May 2022, 2:11 pm

Na;Yussuph Hassan.

Imeelezwa kuwa Shinikizo la juu la damu pamoja na kisukari ni vyanzo vya figo kushingwa kufanya kazi na kusababisha kusambaa kwa sumu mwilini endapo mgonjwa asipopata matibabu kwa wakati.

Akizungumza na kituo hiki Daktari bingwa wa Magonjwa ya figo kutoka Hopsitali ya Benjamini Mkapa Kessy Shijja amesema kuwa kwa Bara la Afrika kwa kiasi kikubwa ugonjwa huo unasababishwa na shinikizo la juu la damu ijapokuwa hivi karibuni pia ugonjwa kisukari umeongezeka.

.

Aidha amesema kuwa ugonjwa huo umegawanyika katika hatua tano huku hatua za awali zikiwa hazioneshi dalili zozote.

.

Wakizungumza na taswira ya habari baadhi ya wakazi mkoani hapa wamesema kwa sasa elimu ya kuimarisha mtindo bora wa maisha pamoja na kupima afya mara kwa mara wameipata, changamoto ni umasikini unaowakabili.

Takwimu za hivi karibuni kutoka wizara ya afya zinaonesha kuwa asilimia kumi ya watu duniani wanaishi na magonjwa sugu ya figo huku asilimia 50 ni watu wenye umri wa miaka 75.