Dodoma FM

Wasichana wahofia kuripoti vitendo vya ukatili

11 May 2022, 2:02 pm

Na;Mindi Joseph.

Imeelezwa kuwa asilimia kubwa ya wasichana hawaripoti vitendo vya ukatili wa kijinsia wanavyofanyiwa kwa kuhofia kudhalilika.

Taswira ya habari imezungumza na Mkaguzi wa polisi Christer yasinta Mkuu wa dawati la jinsia na watoto Polisi Mkoa wa Dodoma ambapo amesema kundi kubwa wanaoripoti ukatili wa kijinsia ni wanawake.

Ameongeza kuwa asilimia kubwa wasichana ndio wamekuwa nyuma kuripoti ukatili wa kijinsia kwa kuogopa kupoteza ndoto zao.

.

Ameongeza kuwa kama dawati la jinsia na watoto wanatamani kuona ukatili wa kijinsia unatokomezwa Kabisa.

Ukatili wa kijinsia kwa wanawake,watoto na wasichana bado unaendelea kufanyika katika maeneo mbalimbali nchini hivyo jitihada za pamoja zinahitajika kutokomeza vitendo hivi.