Dodoma FM

Mazae waendelea kupata changamoto ya maji

6 May 2022, 3:13 pm

Na,Mindi Joseph.

Changamoto ya upatikanaji wa maji bado inaendelea kuwakabili wananchi wa kijiji cha mazae wilayani mpwapwa.

Taswira ya habari imezungumza na Mwenyekiti wa kijiji cha mazae steven Makasi ambapo amesema changamoto hii imekuwepo kwa muda  kirefu.

Ameongeza kuwa wananchi wanalazimika kutembea umbali mrefu ili kufikia huduma ya maji.

.

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Mazae Mwl.William Madanya amesema Mamlaka ya maji vijijini tayari inatekeleza mradi wa maji wenye thamani ya Million 255.

.

Wananchi wamehimizwa kuendelea kuitunza miundombinu ya maji na kuondokana na uharibifu unaofanyika.