Dodoma FM

Wananchi watakiwa kutambua umuhimu wa Mbaazi

5 May 2022, 2:00 pm

Na; Leonard Mwacha.

Wananchi mkoani Dodoma wametakiwa kutambua umuhimu wa zao la mbaazi kuwa lina manufaa makubwa katika matumizi mbalimbali pamoja na biashara.

Wito huo umetolewa na, Mkurugenzi wa  wa asasi siyokuwa ya serikali SEIDA Bw. Fredrick Ogenga, kupitia warsha ya siku 3 iliyoandaliwa na asasi hiyo yenye lengo la kuhamasisha soko la ndani la zao la mbaazi kwenye chakula kama lishe.

Ogenga amesema, wajasiriamali wana nafasi kubwa ya kunufaika kibiashara, endapo wataongeza dhamani  ya zao hilo kwa matumizi mbalimbali.

Aidha, ameitaka jamii kutokuichukulia mbaazi kama chakula cha watu wenye kipato cha chini na badala yake watambue kuwa mbaazi ina faida kubwa kwa binadamu.

Nao baadhi ya washiriki wa warsha hiyo wameeleza watakavyo ongeza dhamani ya zao hilo la mbaazi ili waweze kunufaika zaidi.

.

Asasi ya SEIDA inashirikiana na ,mfuko wa kuendeleza mifumo ya masoko AMDT katika kufanikisha mradi wa kuhamasisha soko la ndani la zao la mbaazi  kwenye lishe na chakula linalolenga kuimarisha  upatikanaji wa lishe linganifu, mapato na ajira kwa vijana na wanawake.