Dodoma FM

Viongozi wa Dini watakiwa kuhamasisha zoezi la sensa

5 May 2022, 7:13 am

Na; Benard Filbert.

Imeelezwa kuwa viongozi wa dini wanayo nafasi kubwa ya kuhamasisha zoezi la sensa na makazi ambalo linatarajiwa kufanyika mwaka huu mnamo mwezi Agosti.

Hayo yameelezwa na baadhi ya wakazi jijini hapa wakati wakizungumza na taswira ya habari kuhusu hamasa kwa wananchi kuelekea kufanyika kwa sensa ya watu na makazi.

Wakazi hao wamesema ili kukamilika kwa zoezi la sensa ni vyema viongozi wa dini wakaendelea kuhamasisha watu katika nyumba za ibada ili kuleta utayari wa jambo hilo pindi muda utapofika.

.

Jana katika sikukuu ya Eid el fitri Sheikh mkuu wa mkoa wa Dodoma Mustafa Rajab wakati akiongoza swala katika msikiti Gadaffi jijini hapa aliwaasa waamini wa dini ya kiislamu kujitokeza katika sensa na makazi zoezi hilo litakapowadia.

.

Mwaka huu mwezi Agosti litafanyika zoezi la sensa ya watu na makazi lengo likiwa kutambua idadi ya watu waliopo nchini huku viongozi mbalimbali wakiendelea kuhamasisha jamii kutoa ushirikiano kwa maafisa wa sensa watakapofika katika kaya zao.