Dodoma FM

Zoezi la chanjo ya polio la ahirishwa hadi may 12 na 15

29 April 2022, 6:48 am

Na;Yussuph Hassan.

Zoezi la chanjo ya ugonjwa polio lililotarajiwa kuanza jana Nchini, limehairishwa ambapo zoezi hilo litafanyika kuanzia mwezi may 12-15 nchini huku wananchi wakikisitizwa kujiandaa na zoezi hilo.

Akizungumza na kituo hiki Mratibu wa Chanjo Mkoani Dodoma Victor Kweka amesema kutoka na sababu mbalimbali zoezi hilo limeahirishwa ambapo linatarajiwa kufanyika mwezi may mwaka huu.

.

Aidha amesema zoezi hilo litafanyika kwa muda wa siku nne na baada ya kumalizika watafanya tathmini namna ya kuendelea kuhudumia kwa watoto waliokosa huduma hiyo.

.

Inakadiriwa Zoezi hilo la Chanjo limekusudia kuchanja Jumla ya watoto  479,156.wenye umri chini ya miaka mitano mkoani Dodoma ambapo wanatarajia kupata chanjo ya matone ya ugonjwa wa Polio ili kuwajengea kinga na kuzuia kuenea kwa Virusi hivyo.