Dodoma FM

Serikali yashauriwa kusimamia malipo kwa wafugaji

22 April 2022, 1:53 pm

Na;Yussuph Hassan.

Serikali Nchini imeshauriwa kusimamia kwa kina suala la malisho kwa wafugaji kwani kundi hilo limekuwa likichangia kwa kiasi kubwa shughuli za kiuchumi.

Akizungumza na waandishi wa habari na Mwenyekiti wa Chama Cha Wafugaji Nchini Jeremia Wambura amesema kuwa suala la malisho kwa wafugaji ni muhimu sana huku wakisuburia sensa ya kutathimini mifugo ili kujua mahitaji ya nchi nzima.

.

Aidha ameshauri Serikali kuwepo kwa sheria rafiki na wazi zisizoathiri shughuli za wafugaji Nchini.

.

Taswira ya habari imezungumza na wafugaji Mkoani hapa ambapo wamesema kuwa ni vyema elimu ikatolewa kwa wafugaji na wakulima ili kudhibiti migogoro ya ardhi nchini.

.

Hapo jana wizara ya mifugo na uvuvi ilikutana na kundi la wafugaji nchini ambapo mh Mashimba Ndaki ameahidi kufanyia kazi changamoto zinawakabili kundi hilo.