Dodoma FM

Serikali kufanyia utafiti jiwe la Ruby lililopo Dubai

22 April 2022, 2:07 pm

Na; Shani Nicolous.

Mara baada ya taarifa zinazosambaa mitandaoni  kuhusu jiwe la Ruby lililopo Dubai Wizara ya madini imesema inafanya utafiti na kutoa majibu sahihi namna taifa litanfaika na jiwe hilo.

Akizungumza bungeni  Naibu waziri wa madini Mh.Dr. Steven Kiruswa kwa niaba ya waziri wa madini amesema kuwa Jiwe hilo lenye uzito wa kilo mbili nukta nane  thamani ya dolla za kimarekani millioni  120 sawa na zaidi ya shilingi billioni 240 za Kitanzania hawana taarifa za ufikaje Dubai kwa madini hayo.

CLIP ….NAIBU WAZIRI.

Amesema kuwa baada ya kufuatilia wakabaini mmiliki wa sasa wa jiwe hilo yupo nchini Marekani katika jimbo la Khalfonia na mawasiliano ya awali yanafanyika ili kuupata ukweli halisi juu ya nchi hizi tatu husika Dubai, Marekani na Tanzania.

CLIP ….NAIBU WAZIRI

Amewahakikishia Watanzania endapo itabainika jiwe hilo ni la Kitanzania nchi itanufaika na mali hiyo bila dhuruma yoyote na Wizara imejipanga vilivo katika hilo.

CLIP ….NAIBU WAZIRI

Baadhi ya wananchi wamesema serikali iongeze umakini kulinda mali za nchi hasa katika kuzitoa nje ya nchi kwani nchi ya Tanzania ni tajiri ila inanufaisha nchi nyingine kwa kukosa umakini.