Dodoma FM

Lugha mama itumike kufundishia shuleni

21 April 2022, 11:05 am

Na; Yussuph Hassan.

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limeendelea leo kwa kujadili hotuba ya bajeti katika Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tamisemi.

Katika kujadili bajeti hiyo Mbunge wa jimbo la Tabora Kaskazini Athumani Almas ameomba Serikali kuangalia kwa kina suala la utumiaji wa lugha ya kiingerereza katika ufundishaji shuleni, huku akisema ili taifa lipate maendeleo kwa haraka ni vyema litumie lugha mama katika ufundishaji.

.

Ameongeza kuwa awali amewahi kuwasilisha muswada wa kubadilisha sera hiyo ya elimu huku kukiwa hakuna mabadiliko na hivi karibuni amezimia kupeleka muswada mwingine.

.

Kwa upande mwengine Mbunge wa Viti Maalum Mh Mwantumu Mzami Zodo ameliongelea kwa uzito wake suala la posho za madiwani huku akishauri serikali kuelekea katika zoezi la sensa ya watu na makazi, Wenyeviti na watendaji wapewe mafunzo katika vyuo vya utumishi.

.

Bunge la 12 mkutano wa saba wa bunge la bajeti kikao cha tisa umeendelea leo jijini Dodoma.