Dodoma FM

Zahanati ya Kisokwe kukamilika punde

12 April 2022, 3:27 pm

Na;Mindi Joseph.

Halmashauri ya wilaya ya Mpwapwa imefanikiwa kupeleka Million 50 za kukamilisha  ujenzi wa  zahanati ya kisokwe wilayani humo.

Taswira ya habari imezungumza na Diwani wa kata ya mazae Mwl Willium Madae amesema pesa hizo zitachangia Ujenzi wa zahanati ya Kijiji cha Kisokwe kukamilika mwezi june na kuondoa adha ya mama wajawazito kupata changamoto wakati wakujifungua.

Ameongeza kuwa kukamilika kwa zahanati hiyo itasaidia kuhudumia takribani vijiji vitatu vinavyozunguka zahanati hiyo.

.

Katika hatua nyingine wananchi wanaendelea na ujenzi wa nyumba ya kuishi ya mganga mkuu wa zahanati hiyo.

.

Baadhi ya wananchi wa Mazae wanasema ni ahueni kubwa kwao pindi itakapokamilika zahati hiyo.

Serikali imepongezwa kwa jitihada inazoendelea kuzifanya kuhakikisha inaboresha zaidi huduma za afya.