Dodoma FM

Serikali idhibiti ongezeko la watoto wa mitaani

12 April 2022, 4:26 pm

Na; Shani Nicolous.

Wakati siku ya mtoto anayeishi na kufanya kazi  mtaani ikiadhimishwa kimataifa serikali imeombwa kuongeza nguvu na itilie mkazo jambo la kudhibiti  ongezeko la watoto wa mtaani.

Akizungumza na kituo hiki Elizabeth Msuya kutoka Taasisi isiyo ya kiserikali ya Focus For The Future Generation amesema juhudi za mashirika yasiyo ya kiserikali pekee haziwezi kumaliza tatizo la ongezeko la watoto wa mtaani , makadilio yanaonyesha si chini ya watoto elfumoja kila mwaka wanakimbilia mtaani.

.

Ameongeza kuwa ni wakati sasa jamii kuamka na kutengeneza urafiki na watoto wao ili kujenga mahusiano bora yatakayotengeneza malezi mazuri ambayo yatafunga milango ya watoto hao kukimbilia mtaani.

.

Amesema kupanga uzazi ni suluhu moja wapo ya kupunguza wimbi hili la watoto wa mtaani ,hivyo dhana potofu juu ya elimu ya afya ya uzazi iachwe ili kuleta mabadiliko katika jamii.

.

Kwa upande wao baadhi ya wananchi jijini hapa wamesema kuwa wazazi watengeneze desturi ya kupanga uzazi kwa pamoja ili kuepuka kuwa na watoto watakaokosa matunzo ,na serikali itenge maeneo kwaajili ya malezi ya watoto hawa.

.

Kila ifikapo april 12 kila mwaka kimataifa huadhimisha siku ya watoto wanaoishi na wanaofanya kazi mtaani ambapo baadhi mashirika nchi hapa huadhimisha siku hiyo kwa kutoa elimu mbalimbali.