Dodoma FM

Elimu ya Saikolojia yaendelea kutolewa kwa jamii

12 April 2022, 3:10 pm


Na;Mindi Joseph.

Asasi ya Saiko Center imeendelea kutoa elimu ya saikolojia ili kuhakikisha inasaidia jamii kuepukana na changamoto za kisaikolojia.

Taswira ya habari imezungumza na Mtendaji wa Asasi hiyo Sylvia Siriwa ambapo amesema malengo yaliyopo kwenye asasi hiyo ni kutoa huduma iliyo bora kwa jamii.

Ameongeza kuwa ili kuifikia zaidi jamii wanaendelea kufanya kazi kwa kushirikiana karibu na asasi zingine zenye mlengo wa kusaidia jamii.

.

Kwa upande wake Furaha Ibaro Mkurugenzi Mtendaji wa Inua Foundation amesema asasi nyingi hazijajikita kusaidia wananchi wanaokabiliwa na changamoto za saikolojia.

.

Nao baadhi ya ya wananchi wamesema jamii kwa kiasi kikubwa bado haina elimu ya saikolijia.

.