Dodoma FM

Wakazi Jijini Dodoma watakiwa kuwa waadilifu juu ya matumizi ya maji

1 April 2022, 2:17 pm

Na;Yussuph Hassan.

Wakazi Jijini Dodoma wameshauriwa kuwa waadilifu katika matumizi ya Maji na kutoa taarifa panapotokea changamoto yoyote ya upatikanaji wa huduma hiyo.

Ushauri huo umetolewa na Meneja Ufundi wa Duwasa Emmanuel Mwakabore wakati  akizungumza na kituo hiki kufatia kuwepo kwa uhaba wa maji mkoani hapa.

Bw. Mwakabore amesema licha ya kuwa Serikali inaendelea kuboresha huduma ya Maji Dodoma, ni vyema Wananchi wakawa waadilifu na kutoa taarifa za hali ya huduma hiyo katika maeneo yao.

Ameongeza kuwa Mamlaka inaangalia maeneo ya karibu ya kupata Maji ili kuendelea kuhudumia Wananchi wa maeneo ya karibu na vyanzo hivyo.

Hivi karibuni Dodoma imekumbwa na upungufu wa maji kutokana na ongezeko kubwa la watu na kusababisha kuwepo kwa mgao wa huduma ya maji maeneo mbalimbali mkoani hapa.