Dodoma FM

Wakazi wa Chang’ombe Ihumwa walalamikia huduma ya Afya kuto kujitosheleza

28 March 2022, 2:48 pm

Na;Neema Shirima.

Baadhi ya wananchi wa mtaa wa chang’ombe kata ya Ihumwa jijini Dodoma wameelezea changamoto zao ikiwa ni pamoja na kutojitosheleza kwa huduma ya afya katika kata hiyo

Wakizungumza na taswira ya habari wananchi hao wamesema kwa sasa ongezeko la watu ni kubwa katika kata hiyo na inawalazimu kutumia zahanati moja iliyopo katika kata hiyo ambapo wameiomba serikali iwasaidie waweze kupata zahanati nyingine ili waweze kupata huduma hiyo

Clip 1……mwananchi

Wamesema inawalazimu kutembea umbali mrefu kufuata huduma ya afya ama kulazimika kwenda katika zahanati binafsi ambapo pia hakuna huduma ya kliniki ya watoto

Aidha mwenyekiti wa mtaa huo bwn Yoram Paulo amesema tayari wameshapeleka ombi la kujengewa zahanati na tayari wametenga zaidi ya hekari kumi kwa ajili ya ujenzi huo na hapa anaeleza zaidi

Ni jukumu la jamii pamoja na serikali kuhakikisha zinashirikiana kwa pamoja katika kuboresha miundombinu ikiwa ni pamoja na huduma bora za afya kwa jamii