Dodoma FM

Uhaba wa madawati bado ni changamoto katika sekta ya elimu

23 March 2022, 2:53 pm

Na ;Victor Chigwada .

Mbali na changamoto ya vyumba vya madarasa pamoja na walimu katika shule za msingi na sekondari lakini uhaba wa madawati nao umeongeza changamoto katika sekta ya elimu   

 Kata ya Mpalanga Wilaya ya Bahi ni miongoni mwa Kata zenye changamoto ya madawati katika shule za msingi na sekondari nakuwalazimu wazazi kuchangia fedha za madawati

Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Nholi Kata ya Mpalanga wamekiri kukabiliwa na changamoto hiyo hivyo kwa sasa wapo katika kuchangishana ili kuondokana na adha hiyo

Mwenyekiti wa kijiji cha Nholi Bw.Lameki Omary amesema kuwa kutokana na upungufu huo wameamua kununua baadhi ya madawati ili kupunguza changamoto hiyo

Naye diwani wa Kata hiyo Bw. Baraka Ndahani amesema kutatua changamoto hiyo mojakwamoja haitakuwa rahisi hivyo wataendelea kupunguza taratibu kutokana na fedha watakayo kusanyakwa wananchi

 Changamoto ya madawati imekuwa kubwa kwa shule nyingi za serikali  kutokana na ongezeko la wanafunzi wanao jiunga darasa la kwanza na kidato cha kwanza kuwa kubwa kwa hivi karibuni