Dodoma FM

Wananchi watakiwa kuitumia[WU1]  kwaresma kutenda matendo ya huruma

22 March 2022, 2:11 pm

Na; Seleman Kodima

Wito umetolewa kwa wananchi kutumia mwezi huu wa mfungo wa kwaresma kutenda matendo ya huruma  kwa jamii ikiwemo kuwajali na kuwapa mahitaji watu wasiojiweza .

Hayo yamesemwa na Vijana wa Kanisa la waadventista wa sabato kutoka kanisa la Dodoma kati wakati wakifanya Usafi katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Dodoma ikiwa ni muendelezo na Matendo ya huruma kwa jamii .

Akizungumza na Dodoma Fm Mwenyekiti wa kamati ya Vijana Kanisani hapo Mack Mori amesema ni Vyema jamii kutumia mwezi huu kama Ishara ya kutenda matendo ya Huruma.

Baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari Dodoma ambao wameshiriki katika shughuli za kijamii wametoa wito kwa jamii kuwa na utamaduni wa kuwatembelea wagonjwa na kuwasaidia watu wasio jiweza .

kwa upande wake Mwakilishi wa Mganga mfawidhi  wa Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Dodoma Mkuu wa Idara ya afya na Mazingira Bw Haule Mgeni amewashukuru vijana hao kwa kitendo walichokifanya kwa kuwakumbuka wahitaji na taasisi muhimu za jamii.

Zoezi hilo  la matendo ya huruma linamebebwa  na Mistari inayotoka katika kitabu cha Mwenyezi Mungu  Biblia tukufu  kitabu cha Yakoco 1;27  kinasema Dini iliyo safi, isiyo na uchafu mbele za Mungu Baba, ndio hii: kuwasaidia yatima na wajane katika dhiki zao, na kujilinda mwenyewe usichafuliwe na ulimwengu.

Na Selemani Kodima