Dodoma FM

Watu wenye ulemavu waomba elimu juu ya umuhimu wa sensa

16 March 2022, 1:57 pm

Na; Mariam Matundu.

Watu wenye ulemavu wameiomba serikali kuwaelimisha juu ya umuhimu wa sense kwa kundi hilo ili waweze kushiriki kikamilifu kuhesabiwa pindi zoezi litakapoanza.

Wakizungumza na taswira ya habari baadhi ya watu wenye ulemavu wamesema sense ni muhimu kundi la watu wenye ulemavu kwa kuwa itasaidia kupata takwimu sahihi zitakazotumika katika mipango mbalimbali.

Bwana Maiko salali ni mwenyekiti wa hope foundation for disabilities amesema bado jamii ya watu wenye ulemavu hawana elimu ya kutosha juu ya umuhimu wa sensa na kwamba ni muhimu pia kuandaa miundombinu itakayowezesha kundi hili kuhesabiwa bila vikwazo.

Kwa uande wake katibu wa shirikisho la vyama vya watu wenye ulemavu SHIVYAWATA amesema anaona dalili nzuri za ushiriki wa watu wenye ulemavu kwakuwa tayari uwakilishi wa watu wenyeulemavu upo katika kamati ya sense ya mkoa.

Kilio cha Takwimu sahii za watu wenyeulemavu kimekuwa cha muda mrefu kwa wadau na Kwa mujibu wa sense ya watu na makazi ya  mwaka 2012 watu wenyeulemavu ni takribani milioni tatu ambapo mwaka huu inatarajiwa kufanyika sense ya watu na makazi .