Dodoma FM

Wakazi wa mtaa wa Chang’ombe Ihumwa walalamikia kukosa huduma ya maji

10 March 2022, 3:46 pm

Na; Neema Shirima.

Baadhi ya wananchi wa mtaa wa Chang’ombe kata ya Ihumwa jijini Dodoma wameelezea changamoto zao ikiwa ni pamoja na ukosefu wa maji safi na salama katika eneo hilo

Wamesema ukosefu wa maji safi na salama unawalazimu kutumia maji ya visima ambayo sio salama kwao na kuiomba serikali iwaboreshee miundo mbinu ya maji ili waweze kuondokana na changamoto hiyo

Wamesema idara ya maji Mkoa wa Dodoma DUWASA waliwaahidi kuwatatulia changamoto hiyo lakini hadi sasa bado hawajafanya hivyo na kuwaomba kuitimiza ahadi yao ili waweze kupata huduma hiyo

Aidha mwenyekiti wa mtaa huo bwn Yoram Paulo amekiri kuwepo kwa changamoto hiyo ambapo amesema tayari wameshasambaza mabomba lakini bado hawajaweka tanki la kuhifadhia maji na kuiomba serikali iwawekee tank la kuhifadhia maji ili iwe rahisi kusambaza maji kwa wananchi na kuondokana na changamoto hiyo

Kila jamii inatakiwa kutumia maji safi na salama ili kuondokana na magonjwa ya mlipuko kama vile kipindupindu hivyo ni jukumu la serikali kuhakikisha kila jamii inapata huduma ya maji safi na salama.