Dodoma FM

TBA yatakiwa kuharakisha mchoro wa jengo la ofisi

10 March 2022, 2:38 pm

Na; Mariam Matundu.

Katibu mkuu wizara ya maendeleo ya jamii ,jinsia ,wanawake na makundi maalumu Dkt Zainabu Chaula amewaomba wakala wa majengo ya serikali (TBA) kuharakisha taratibu za kupata mchoro wa jengo la ofisi za wizara hiyo ili ujenzi uanze mapema .
Dkt Chaula ametoa kauli hiyo wakati akipokea kiwanja kwa ajili ya ujenzi wa ofisi ya wizara katika mji wa serikali mtumba tangu kuundwa kwa wizara hiyo mpya ambapo awali ilikuwa ni sehemu ya wizara ya Afya.
Amesema TBA ifanye jukumu lake la kuhakikisha mchakato wa ujenzi unakamilika kwa wakati hivyo kuwezesha wizara kuendelea kuhudumia wananchi kwa sababu inagusa makundi yote katika jamii ikiwemo makundi maalumu.
Clip 1 katibu mkuu……………..
Kwa upande wake mratibu wa ujenzi wa mji wa serikali Meshack Bandawe amesema kutokana na mahitaji ya wizara hiyo kwa ukubwa wake kulikuwa na umuhimu kuwa na eneo lake na jengo kamili ili kurahisisha shughuli zake ili kukidhi mahitaji ya seriakali kwa miaka ijayo.
Clip 2 mratibu……………………
Ngh’olo Weja ni msanifu wa majengo kutoka TBA amesema kuwa watahakikisha mchoro wa majengo hayo unakamilika mapema kwa kufuata sheria pamoja na taratibu zote za kumpata mkandarasi.
Clip 3 msanifu ……………….