Dodoma FM

Wakazi wa Mkoka waiomba serikali kukamilisha mradi wa maji

1 March 2022, 3:53 pm

Na; Victor Chigwada.

Wananchi wa kata ya Mkoka Wilaya ya kongwa wameiomba Serikali kukamilisha miradi ya maji safi ili waweze kuondokana na changamoto hiyo ya muda mrefu

Wakizungumza na taswira ya habari baadhi ya wananchi hao wamesema ukosefu wa maji unawafanya kutumia maji ya korongoni kutokana na kisima chao kuharibika muda mrefu

Mwenyekiti wa kijiji cha Mkoka Bw.Elia Chibago amekiri kisima cha maji kilishindwa kufanya kazi kutokana na ubovu wa miundombinu hivyo kupelekea adha kwa wananchi

Naye Diwani wa Kata hiyo Bw.Richadi Mwite amesema kwa baadhi ya vijiji walipata msaada kutoka world Vision kwa kuwachimbia visima ila changamoto kubwa imebaki kijiji cha mkoka ambacho nacho tayari kimechimbiwa visima vitatu ambavyo bado havija kamilika

Shirika la World Vision nchini limekuwa karibu na wananchi hasa katika utatuzi wa changamoto za huduma za kijamii ikiwa ni pamoja na uchimbaji wa visima vya maji