Dodoma FM

Zoezi la uchukuaji wa miti katika ofisi za maliasili litekelezwe na kila mwananchi

16 February 2022, 3:43 pm

Na; Thadei Tesha.

Wananchi jijini Dodoma wamewataka viongozi wa mitaa mbalimbli jijini hapa kuendelea kuhamasisha kufika katika ofisi za maliasili kuchukua miche ya kupanda katika maeneo yao

Wakizungumza na taswira ya habarri baadhi ya wananchi jijini hapa wamesema ni wakati wa viongozi wa mitaa pamoja na taasisi mbalimbali ikiwemo shule na viongozi wa dini kuendelea kuhamasisha zaidi kuhusiana na suala hilo pale wanapokutana na jamii katika majukumu yao.

Kwa upande wao baadhi ya viongozi wa mitaa pamoja na taasisi za dini wamesema wataendelea kuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha wananchi kuhusiana na umuhimu wa kupanda miti hususani katika kipindi hiki cha mvua ili kuendelea kuunga mkono sera ya taifa ya mazingira ya mwaka 2021.

Hivi karibuni afisa maliasili wa jiji la dodoma Bw Vedasto Mlinga wakati akizungumza na taswira ya habari aliwataka wananchi kufika katika ofisi za maliasili zilizopo katika halmashauri ya jiji kwa lengo la kupata miche ya miti watakakayoipanda katika maeneo yao.

Suala la kupanda miti limeendelea kusisitizwa na viongozi mbalimbali wa serikali na taasisi mbalimbali ambapo lengo kubwa ni kuhakikisha mandhari ya jiji inaendelea kuwa ya mvuto pamoja na kuzuia athari za uharibifu wa mazingira.