Dodoma FM

Wananchi waomba kupatiwa elimu juu ya mazoezi ya viungo

15 February 2022, 4:42 pm

Na ;Thadei Tesha.

Mwitikio wa watu kufanya mazoezi bado umeendelea kuwa wa wastani kutokana na watu kutopata elimu ya kutosha juu ya umuhimu wa kufanya mazoezi.

Taswira ya habari imefanya mahojiano na wananchi jijini hapa kufahamu ni kwa kiasi gani  wamekuwa wakifanya mazoezi pamoja na kuzingatia suala la mlo kamili .

Baadhi ya wananchi jijini hapa wamesema ipo haja kwa taasisi za afya kuendelea kutoa elimu pamoja na kuhamasisha wananchi kuhusiana na umuhimu wa watu kufanya mazoezi pamoja na kuzingatia mlo kamili ili kuepukana na magonjwa mbalimbali ikiwemo presha na shinikizo la damu.

Kwa upande wake mtaalamu wa afya kutoka katika hospitali ya Ocean Road jijini hapa amesema ili kupunguza watu kupata magonjwa yatokanayo na kushindwa kufanya mazoezi ni wakati kila mtu kuanza kufanya mazoezi binafsi ambapo amesema sio kukimbia pekee bali pia kila mmoja anaweza kufanya hata akiwa chumbani kwake.

Suala la kufanya mazoezi limekuwa likihimizw katika jamii kwa kiasi kikubwa ambapo lengo lake ni kupunguza kupata magonjwa mbalimbali ikiwemo shinikizo la damu.