Dodoma FM

Wakazi wa Chitabuli waomba kujengewa Zahanati

14 February 2022, 5:44 pm

Na; Neema Shirima.

Wananchi wa kijiji cha Chitabuli katika kata ya Membe jijini Dodoma wameiomba serikali iwajengee zahanati ili waweze kuondokana na changamoto ya ukosefu wa huduma hiyo katika kijiji hicho

Wakizungumza na taswira ya habari wananchi hao wamesema changamoto ya ukosefu wa zahanati kunapelekea kuhatarisha maisha ya mama wajawazito wanapofikia kujifungua kwani inawalazimu kutembea umbali mrefu kwa ajili ya kufata huduma ya afya

Wamesema wao wamejitolea kwa kuchangishana na kufyatua tofali hivyo wanaiomba serikali iwasaidie katika ujenzi huo ambao tayari wameuanzisha

Aidha mwenyekiti wa kijiji hicho Bw Keneth Paulo amekiri kuwepo kwa changamoto hiyo ambapo amesema baadhi ya wajawazito hulazimika kujifungulia nyumbani bila kuwepo na wataalamu hali inayopelekea hatari ya maisha ya mama na mtoto

Afya ni suala la msingi katika maisha ya binaadamu hivyo ni wajibu wa jamii pamoja na serikali kuhakikisha huduma hiyo inapatikana ili kunusuru maisha ya wananchi.