Dodoma FM

Sera ya Taifa ya mwaka 2021 yazinduliwa

14 February 2022, 5:54 pm

Na; Thadei Tesha.

Kufuatia hivi karibuni mkamu wa Rais Mh Philip Mpango kuzindua sera ya taifa ya mazingira ya mwaka 2021 jijini hapa baadhi ya wananchi jijini hapa wameipongeza serikali kwa kuendela kuhamasisha suala la utunzaji wa mazingira katika jamii.

Wakizungumza na taswira ya habari wananchi jijini hapa wamesema ni wakati wa kila mwananchi kuunga mkono sera hiyo kwa vitendo kwa kila mmoja kuwa stari wa mbele katika kupanda miti kutokana na miti hiyo kutolewa bure na serikali ikiwa ni pamoja na kufanya usafi wa mazingira.

Aidha kwa upande wao baadhi ya wauzaji wa miche ya miti na maua wameishukuru serikali kwa kuzindua sera hiyo ambapo itawahamasisha kupanda miti kwa wingi kutokana na wateja kuanza kuongezeka kwa ajili ya kununua miti hiyo.

Wakati akizindua sera ya taifa ya mazingira ya mwaka 2021 katika viwanja vya Nyerere square hivi karibuni makamu wa rais alitoa wito kwa wananchi kuendelea  kutunza mzingira ikiwa ni pamoja na kupanda miti ambapo pia aliwataka wananchi jijini hapa kuacha kukata miti hovyo.

Kauli mbiu ya uzinduzi wa sera’ hiyo ni mimi natekeleza sera ya taifa ya mazingira’ ambapo lengo lake ni kuhakikisha  mazingira ya miji yanakuwa safi ikiwa ni pamoja na jiji la Dodoma  ambapo wananchi wameendelea kuhamasishwa kupanda miti pamoja na kutunza mazingira.