Dodoma FM

Ukosefu wa chakula shuleni wapelekea wanafunzi kutofanya vizuri

8 February 2022, 4:45 pm

Na; Neema Shirima.

Hali ya ukosefu wa chakula kwa wanafunzi katika baadhi ya shule za msingi jijini Dodoma inachangia wanafunzi kutofanya vizuri darasani pamoja na utoro

Akizungumza na taswira ya habari mwalimu mkuu msaidizi wa shule ya msingi Chitabuli iliyopo katika kata ya Membe jijini Dodoma mwalimu Salina Ng’umbi amesema wazazi hawana mwamko wa kuchangia chakula kwa ajili ya watoto wawapo shuleni hali ambayo inawafanya baadhi ya wanafunzi kusinzia kutokana na njaa ama kutofika kabisa darasani.

Aidha mwenyekiti wa kijiji hicho amesema elimu kuhusu uchangiaji wa chakula cha wanafunzi imetolewa kwa wazazi lakini bado elimu hiyo haijazaa matunda

Kwa upande wa wazazi wamesema hali ya kutokuchangia chakula ni uelewa mdogo wa baadhi ya wazazi ambapo wamesema wataelimishana ili waweze kuanza uchangiaji huo

Jamii inashauriwa kushirikiana na waalimu ili kuhakikisha  wanafunzi wanapata haki zao za msingi ikiwa ni chakula kwa wakati pamoja na kusoma katika mazingira yatakayowawezesha kufurahia wanachokipata kutoka kwa waalimu wa