Dodoma FM

Vyombo vya sheria vyaombwa kusimamia haki

7 February 2022, 3:44 pm

Na; Benard Filbert.

Vyombo vinavyosimamia sheria nchini vimeombwa kusimamia haki pale inapobainika mtu yeyote kufanya vitendo vya kikatili ili kukomesha  hali hiyo.

Hayo yamebeinishwa na afisa miradi Bi Stella Matei kutoka taasisi ya ACTION FOR COMMUNITY CARE ambayo inajihusisha na kutoa elimu kwa jamii kuhusu ukatili wa kijinsia.

Amesema licha ya elimu abayo inatolewa na wadau mbalimbali bado kuna vitendo vya ukatili vinaendelea kuripotiwa hivyo ni vyema vyombo husika vikaongeza nguvu kusimamia sheria hizo ili haki itendeke.

Amesema taasisi hiyo imeweza kuyafikia makundi mbalimbalia katika kutoa elimu ambapo wameanza katika shule 12 zilizopo jijini Dodoma ili kuwatengenezea misingi bora ya baadaye.

Baadhi ya wananchi jijini hapa wamesema ili kukomesha vitendo hivyo ni vyema sheria zikachukuliwa kwa wale wanaobainika kwani vitendo vya ukatili havina nafasi katika jamii.

Hivi karibuni kumekuwepo na vitendo vya kikatili katika maeneo mbalimbali nchini huku baadhi ya vitendo hivyo vikisababisha mauaji na kuleta picha mbaya katika jamii.