Dodoma FM

Vijana wahitaji elimu zaidi juu ya madhara ya  matumizi ya pombe na tumbaku

7 February 2022, 2:49 pm

Na; Thadei Tesha.

Baadhi ya vijana jijini hapa wamesema elimu zaidi inahitajika kwa vijana ambao wamekuwa wakiathiriwa na matumizi ya pombe pamoja na tumbaku juu ya athari za kiafya zinazoweza kuwapata.

wakizungumza na taswira ya habari baadhi ya vijana jijini hapa wamesema nguvu zaidi bado inahitajika katika kutoa elimu kuhusiana na suala hilo kwani vijana wengi wamekuwa wakitumia bila ya kujua athari zake.

Mtaalamu wa magonjwa ya saratani kutoka katika hospitali ya saratani ya Ocean Road amesema vijana wengi ambao wamekuwa wakitumia pombe  na tumbaku wamekuwa wakiripotiwa kupata magonjwa ya saratani kwa kiasi kikubwa .

Aidha amewataka vijana kuachana na matumizi ya pombe na badala yake kuzingatia mazoezi pamoja na lishe bora ili kuepuka na maganjwa mbalimbali ikiowemo saratani ambayo ni miongoni mwa magonjwa yanayoleta madhara makubwa katika jami.

Baadhi ya vijana wamekuwa wakiathiriwa na matumizi ya pombe na tumbaku ambapo wengi wao wamekuwa wakitumia bila ya kufahamu athari zake kiafya ambapo elimu juu ya suala hilo imekuwa ikisisitizwa kutiliwa mkazo katika jamii.