Dodoma FM

Ubovu wa barabara Chitabuli wapelekea akina mama wajawazito kujifungulia njiani

7 February 2022, 4:26 pm

Na; Neema Shirima.      

      

Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Chitabuli kilichopo katika wilaya ya Chamwino jijini Dodoma wameiomba serikali iwaboreshee miundombinu ya barabara ambayo imekuwa ni changamoto kubwa kwao.

Wakizungumza na taswira ya habari wananchi hao wamesema ubovu wa barabara unapelekea baadhi ya kina mama wajawazito kujifungulia njiani wakati wakipelekwa hospitalini kwa ajili ya kujifungua hali inayohatarisha maisha ya mama na mtoto

Aidha mwenyekiti wa kijiji hicho ndugu Keneth Paulo amekiri kuwepo kwa changamoto hiyo ambapo amesema tayari wameshaanza ujenzi wa barabara lakini kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha zoezi limesitishwa hadi itakapoisha

Amesema changamoto hiyo inawaathiri wananchi wa kijiji hicho kwa kiasi kikubwa kwani ndiyo barabara kuu wanayoitumia hasa wakivuna mazao na kutaka kuyasafirisha kwenda kuyauza mjini

Miundo mbinu ya barabara ni jambo la kuzingatiwa hivyo jamii pamoja na serikali wanao wajibu wa kuzingatia uboreshaji wake