Dodoma FM

Wakazi wa Zuzu waomba serikali iboreshe miundombinu ya barabara.

2 February 2022, 4:20 pm

Na; Neema Shirima.

Wananchi wa mtaa wa Pinda katika kata ya Zuzu jijini Dodoma wameiomba serikali iwaboreshee miundombinu ya barabara katika mtaa huo .

Wamesema hali ya barabara hasa kwa kipindi cha mvua imekuwa changamoto kwani wakati mwingine wanashindwa kupita kuelekea mjini kutokana na barabara kuwa mbovu na kutokupitika kwa urahisi

Wamesema mara nyingi barabara hiyo huwa inachongwa lakini kipindi cha mvua inaharibiwa na magari makubwa na kuongeza kwamba lipo gari moja tu kwa siku ambalo huwa wanalitegemea kuelekea mjini ambako ndipo mahitaji yao mengi yalipo

Aidha mwenyekiti wa mtaa huo bwn Salvatori Ole Saitabaho amekiri kuwepo changamoto hiyo ambapo amesema tayari ipo kwenye mkakati wa kujengwa kwa kiwango cha lami

Mtaa wa Pinda ni mtaa uliopo katika kata ya Zuzu jijini Dodoma ambao ni kilomita 11 tu hadi kufika Fourways ambapo wakazi wa mtaa huo wanakabiliwa na changamoto ya miundombinu mibovu ya barabara