Dodoma FM

Jamii yatakiwa kutambua ugonjwa wa ukoma unaambukizwa kwa njia ya hewa

27 January 2022, 3:24 pm

Na; Pius Jayunga.

Jamii imetakiwa kutambua kuwa ugonjwa wa ukoma unaambukizwa kwa njia ya hewa na hivyo kuna haja ya kuchukua tahadhari ikiwemo kuongeza mzunguko wa hewa katika makazi.

Mratibu wa ukoma kutoka wizara ya afya Dr. Dues Kamara ameyasema hayo wakati wa mahojiano na kituo hiki kupitia kipindi cha morning power.

Amesema ni muhimu kujenga nyumba zenye madirisha mkabwa ili kurahisha mzunguko wa hewa, kufunika kinywa wakati wa kupiga chafya pamoja na kuepuka kukaa kwenye maeneo yenye msongamano wa watu.

Amesema hadi sasa haijapatikana chanjo ya kutibu ugonjwa huo licha ya kuwepo kwa chanjo aina ya BSG inayosaidia kuzuia maambukizi ya kifua kikuu mwilini.

Ameasema kuna matumaini makubwa ya kuutokomeza ugonjwa wa ukoma chini kutokana na viashiria mbalimbali vilivyopo ikiwemo kupungua kwa idadi ya watoto wanaobainika kuwa na tatizo hilo.