Dodoma FM

Serikali imesema inatambua mchango unaofanywa na vijana wajasiriamali

25 January 2022, 4:27 pm

Na; FRED CHETI.               

Serikali imesema kuwa inatambua mchango unaofanywa na kundi la vijana wajasiriamali wadogo maarufu kama Machinga katika kukuza uchumi wa nchi huku ikiahidi kutoa ushirikiano wa dhati kwa kundi hilo.

Kaulu hiyo imetolewa leo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassani katika Ikulu jijini  Dar es Salaam alipokutana na kufanya Mazungumzo na viongozi wa Wamachinga pamoja na viongozi wengine Mkoani humo.

Hapa Mh. Rais anaelezea umuhimu wa kundi hilo pamoja na mikakati ya serikali katika kuimarisha zaidi ushirikiano baina ya kundi hilo na serikali .

Wajasiriamali hao wadogo maarufu kama machinga walikuwa na yapi ya kumueleza Mh. Rais? Bw Yusuph Namoto mwenyekiti wa Machinga kwa Mkoa wa Dar esSalaam hapa anazungumza kwa niaba ya wamachinga

Ni utaratibu ambao Mh rais Samia Suluhu Hassani amejiwekea tangu aingie madarakani wa kukutana na makundi mbalimbali na kusikiliza changamoto, maoni pamoja na mapendekezo yao.