Dodoma FM

Msemaji wa jeshi la Zimamoto Nchini aitembelea kampuni ya Dodoma media Group

25 January 2022, 4:59 pm

Na; Mariam Kasawa

Msemaji wa Jeshi la zima moto na uokoaji Nchini SACF Puyo Nzalayaimisi hii leo ameitembelea kampuni ya Dodoma media group inayomiliki vyombo vya habari  vya Dodoma Fm pamoja na Dodoma Tv ili kujionea shughuli mbalimbali za utoaji huduma ya habari.

Msemaji huyo pia amepata wasaa wa kualikwa katika kipindi cha Morning Power cha Dodoma Tv ambapo ametoa elimu kwa wananchi kuhusu kazi za jeshi la zimamoto na uokoaji.

Akizungumza katika kigoda cha Morning Power SACF Nzalayaimisi amesema wananchi wanapaswa kuelewa kuwa wanapo pata majanga ya moto wanapaswa kupiga namba 114 ili kupata msaada wa haraka zaidi kutoka  jeshi la zima moto na uokoaji.

Aidha amewaasa wananchi wenye tabia ya kujiunganishia umeme bila kufuata utaratibu kuacha tabia hiyo kwani ni hatari na inaweza kusababisha majanga ya moto kwa urahisi.

Akizungumzia ushirikiano uliopo kati ya jeshi la zimamoto na Taasisi zingine amesema wamekuwa wakishirikiana vema hasa yanapotokea majanga ili   kutatua na kutoa elimu kwa pamoja .

Amewataka wananchi kutoa taarifa mapema linapotokea janga la moto kwa kupitia namba 114 ili kupata msaada wa haraka kutoka zimamoto .