Dodoma FM

Msitu wapelekea wakazi wa Ihumwa kuishi kwa Mashaka

24 January 2022, 3:45 pm

Na; Neema Shirima.

Baadhi ya wananchi wa mtaa wa chang’ombe kata ya Ihumwa jijini Dodoma wameelezea changamoto wanazokutana nazo katika msitu unaowatenganisha kati ya mtaa wa chang’ombe na mtaa wa mahoma makulu.

Wakiongea na taswira ya habari wananchi hao wamesema kuwa ktika msitu huo mwanzoni yalikua ni mashamba ya watu wakiwa wanalima lakini baadaye jeshi la wananchi wakawakataza kulima kwa madai ya kwamba ni eneo la jeshi ambapo hakuna kinachofanyika zaidi pamegeuka kuwa msitu ambao watu hufanyiwa vitendo vya kikatili kama vile kubakwa na kuuwawa na watu wasiojulikana

Wamesema mara kadhaa hua wanakuta miili ya kina mama ambao wanakua wameuwawa na wengine kuokotwa wakiwa wana hali mbaya na hivyo kuwapeleka hospitali kupatiwa matibabu ambapo wameiomba serikali iwasaidie waweze kuondokana na changamoto hiyo

Aidha mwenyekiti wa mtaa huo ndg Yoram Paulo amekiri kuwepo kwa changamoto hiyo ambapo amesema hadi sasa idadi ya watu sita waliuwawa na watatu waliokotwa wakiwa majeruhi katika pori hilo

Mficha maradhi kifo humuumbua ni msemo ambao wengi hupenda kuutumia na ndivyo ambavyo wakazi wa mtaa wa Chang’ombe kata ya Ihumwa wameamua kupaza sauti zao kuhusiana na changamoto waliyo nayo ya watu kufanyiwa matendo ya kikatili katika msitu uliopo karibu na mtaa wao