Dodoma FM

DUWASA kufichua waharibifu wa miundombinu ya maji

24 January 2022, 3:30 pm

Na; Benard Filbert.

Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira jijini Dodoma DUWASA inaendelea na kampeni yake ya kufichua waharibifu wa miundombinu ya maji ili kukomesha vitendo hivyo.

Hayo yanajiri kufuatia kuwepo kwa uharibifu wa baadhi ya miundombinu ya mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira jijini hapa ikiwepo wizi wa mita za maji.

Sebastian Warioba ni afisa uhusiano wa mamlaka hiyo ameiambia taswira yahabari kuwa  wamelazimika kuanzisha kampeni hiyo ili kuongeza taarifa za watu kufichua vitendo vya uharibifu ambavyo havikubaliki.

Kadhalika amesema kubainika kwa wahalifu hao kunaenda sambamba na ushirikiano wa viongozi mbalimbali wa Kata hadi ngazi ya Mtaa.

Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira jijini Dodoma DUWASA mwishoni mwa mwaka jana ilianzisha kampeni ya kufichua wezi na waharibifu wa miundombinu ya mamlaka hiyo ili kuzuia hasara.