Dodoma FM

Kisedete kupambana na familia zinazo ruhusu watoto kuingia mtaani

20 January 2022, 4:47 pm

Na; Benard Filbert.

Shirika la KISEDET ambalo linajighulisha na kuwahudumia watoto wanaofanya kazi mtaani wamesema mwaka huu watajikita zaidi na familia zinazoruhusu watoto kuingia mtaani ili kukomesha hali hiyo.

Hayo yameelezwa na Ibrahim Mtangoo Afisa ustawi wa jamii kutoka shirika hilo wakati akizungumza na taswira ya habari kuhusu mkakati wa shirika hilo kwa mwaka 2022.

Amesema mkakati uliopo mwaka huu shirika hilo litajihusisha zaidi na familia ambazo zinawaruhusu watoto kuingia mtaani pasipo sababu za msingi hali inayosababisha watoto hao kuendelea kubaki mtaani.

Hata hivyo amesema kwa kiwango kikubwa katika mkoa wa Dodoma wazazi wamekuwa wakiwaacha watoto wajilee wenyewe kitu ambacho ni hatari kwao.

Baadhi ya wazazi wamesema ni vyema kila mmoja akasimama imara ndani ya familia kuhakikisha wanatoa malezi bora kwa watoto.