Dodoma FM

Wakazi wa Ihumwa walalamikia ukosefu wa maji safi na salama

19 January 2022, 3:10 pm

Na; Neema Shirima.

Baadhi ya wananchi wa mtaa wa Chang’ombe kata ya Ihumwa jijini Dodoma wameelezea changamoto ya ukosefu wa maji safi na salama katika eneo hilo

Wamesema ukosefu wa maji safi na salama unawalazimu kutumia maji ya visima ambayo sio salama kwao na kuiomba serikali iwaboreshee miundo mbinu ya maji ili waweze kuondokana na changamoto hiyo

Wamesema idara ya maji Mkoa wa Dodoma yaani DUWASA waliwaahidi kuwatatulia changamoto hiyo lakini hadi sasa bado hawajafanya hivyo na kuwaomba kuitimiza ahadi yao ili waweze kupata huduma hiyo

Aidha mwenyekiti wa mtaa huo bwn Yoram Paulo amekiri kuwepo kwa changamoto hiyo ambapo amesema tayari wameshasambaza mabomba lakini bado hawajaweka tanki la kuhifadhia maji na kuiomba serikali iwawekee tanki la kuhifadhia maji ili iwe rahisi kusambaza maji kwa wananchi na kuondokana na changamoto hiyo

Maji ni uhai kwa kila kiumbe hivyo ni vyema kuhakikisha kila binaadamu na kiumbe hai kinapata huduma hiyo ili kunusuru uhai wake