Dodoma FM

Wazazi watakiwa kuwaandikisha watoto kujiunga kidato cha kwanza.

12 January 2022, 2:20 pm

Na; Benard Filbert.

Wazazi katika kata ya Mbalawala jijini Dodoma wametakiwa kuwaandikisha watoto wao kujiunga kidato Cha kwanza.

Hayo yanajiri kufuatia baadhi ya wanafunzi kudaiwa kuto kuendelea na elimu ya secondari kutokana na sababu mbalimbali.

Ally Mohamed ni Diwani wa kata ya Mbalawala amesema licha ya wanafunzi wengi kufaulu kujiunga na elimu ya sekondari bado kuna changamoto hivyo ni vyema wazazi wakawahamasisha watoto kusoma.

Amesema mwaka huu shule ya sekondari Mbalawala inategemea kupokea zaidi ya wanafunzi 180 kidato cha kwanza.

Amewataka wazazi kuhakikisha wanawapeleka watoto wao shuleni pasipokuwa na kisingizio chochote kwani hivi sasa elimu inatolewa bure.

Serikali imekuwa ikihamasisha wazazi kuhakikisha wanawapeleka watoto shuleni ili wapate elimu.