Dodoma FM

Mlowa bwawani waiomba serikali kuwajengea kituo cha polisi

12 January 2022, 2:34 pm

Na; Neema Shirima.

Wakazi wa kata ya Mlowa bwawani jijini Dodoma wameelezea ushiriki wao katika suala la ulinzi na usalama katika mtaa wao ambapo wamesema wanashiriki vema katika kuhakikisha hali ya ulinzi inakuwepo katika maeneo yao.

Wakizungumza na taswira ya habari wananchi hao wamesema wao wenyewe wanahakikisha wanashirikiana katika suala la ulinzi na usalama ambapo wamefanikiwa kukomesha tatizo la wizi katika eneo hilo

Wamesema mbali na ulinzi wa wao wenyewe bado wanahitaji msaada zaidi wa jeshi la polisi ambapo wameiomba serikali iwajengee kituo cha polisi katika eneo hilo

Aidha diwani wa kata hio bw. Andrew Mseya amesema amefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuanzisha kikundi cha sungusungu ambacho kimewasaidia wananchi kuwa na usalama wa mali zao

Jamii inakumbushwa kuwa wa kwanza  kuhakikisha wanashiriki ulinzi shirikishi katika maeneo yao ili kutokomeza matukio ya kihalifu