Dodoma FM

Zoezi la kuchukua fomu za uspika wa Bunge laendelea

11 January 2022, 2:14 pm

Na; Fred Cheti.

Zoezi la uchukuaji wa fomu kwa ajili ya kugombea kiti cha uspika wa bunge la Tanzania unaendelea ambapo baadhi ya viongozi na watu mbalimbali wameendelea kujitokeza katika zoezi hilo .

Ni Katika makao makuu ya chama cha mapinduzi jijini Dodoma ambapo Dodoma tv ilifika na kukuta zoezi hilo likiendelea huku wagombea wa kiti hicho wakijinadi mbele ya wanahabari juu ya uwezo wao.

Yapi maoni ya wananchi juu ya utaratibu huo katika mchakato wa kumpata mrirthi wa Ndugai je nini Mataminio yao kuhusu kiongozi huyo wa chombo ambacho ni moja kati ya mihimili mikubwa kwa Taifa ?

Mchakato huu unajiri ikiwa zimepita siku kadhaa baada ya Aliyekua spika wa bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Job Ndugai kuachia ngazi katika nafasi hiyo.