Dodoma FM

Chuo cha ufundi stadi chatarajiwa kujengwa Mlowa bwawani.

11 January 2022, 2:08 pm

Na; Neema Shirima.

Serikali ya Tanzania imepokea mradi wa kujenga chuo kikubwa cha ufundi stadi ambacho kitajengwa katika kata ya Mlowa bwawani ndani ya jiji la Dodoma

Hayo yamebainishwa na diwani wa kata hio bwn Andrew ambapo amesema nchi ya Tanzania imepokea mradi huo mwaka jana kutoka serikali ya China ambapo mradi huo ukikamilika utakua msaada mkubwa kwa vijana wa kata hiyo na nchi nzima kwa ujumla

Amesema serikali ya mtaa ya mlowa bwawani imetenga zaidi ya hekari mia moja na hamsini kwa ajili ya ujenzi wa chuo hicho na amewataka wananchi wake wajiandae kupokea mradi huo

Ameongeza kuwa zoezi hilo la ujenzi wa chuo lilitakiwa lianze mwaka jana lakini kutokana na janga la korona kuiathiri nchi ya China kwa kiasi kikubwa likasitishwa ambapo wanategemea kuanza kwa shughuli hii mwaka huu

Maandiko matakatifu yanasema mshike sana elimu usimwache aende zake na hii inathibitishwa na serikali ya Tanzania ambapo bado inaonyesha juhudi katika kuhakikisha vijana wanapata elimu kwa wakati sahihi