Dodoma FM

Tanzania yatakiwa kuwa na sera madhubutu ya nishati jadidifu

17 December 2021, 3:05 pm

Na ;Mindi Joseph.

Jukwaa la wadau wa nishati endelevu limesema Tanzania inahitaji sera madhubutu ya nishati jadidifu nyenye nyezo za utekelezaji katika mageuzi ya matumizi ya nishati na kuongeza usalama na upatikanaji wa nishati Nchini.

Mkurugenzi Mtendaji wa TaTEDO Eng. Estomih Sawe amesema sera ya Taifa ya Nishati ya mwaka 2015 bado haijajipambanua kwa uwazi ili kushughulikia changamoto ya nishati ya kupikia.

Sera hiyo inatoa fursa ya kufanya mageuzi ya kupata suluhisho la changamoto ya nishati ya kupikia ambayo ni jumuishi na endelevu na Kuhama katika matumizi ya mkaa na kutumia Nishati.

Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu, Felchesmi Mramba, amesema Serikali kupitia Wizara ya nishati inaendelea kuhamisisha matumizi ya nishati Jadididfu ambayo vyanzo vyake ni endelevu na rafiki wa mazingira.

Aidha Nishati ya Makaa ya Mawe inatarajiwa kuchangia kwa asilimia 26.7 kutoka asilimia 0 iliyopo kwa sasa na kukinzana na malengo ya sera

Jukwaa la wadau wa nishati endelevu Lililenga kujadili changamoto za kisera katika sekta ya nishati na linahitimishwa leo ijumaa jijini Dodoma.