Dodoma FM

Rais Samia kuunda wizara itakayo shughulikia masuala ya jinsia

16 December 2021, 2:12 pm

Na; Mariam Matundu.

Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema ili kutekeleza kikamilifu ahadi za nchi kuhusu kizazi chenye usawa ataunda wizara maalumu itakayo shughulikia masuala ya jinsia .

Rais samia amesema hayo katika uzinduzi wa kamati ya ushauri ya kitaifa kuhusu utekelezaji wa ahadi za nchi kwenye jukwaa la kizazi chenye usawa ambapo amesema hatua hiyo itasaidia usimamizi na utekelezaji wa sheria,sera na mipango ya uwezeshaji wanawake .

Aidha amesema kamati hiyo ni muhimu ili kuiwezesha Tanzania kuwa kinara katika eneo la haki na usawa wa kiuchumi ni muhimu wakasimamie ,kuratifu na kufanya tathimini katika utekelezaji wake.

Nae waziri mkuu wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Majaliwa Kassimu Majaliwa amesema uzinduzi wa jukwaa hilo kutaongeza chachu ya kufikia malengo ya kizazi chenye usawa .

kwa ubande wake waziri wa afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto Dorothy Gwajima amempongeza Rais Samia kwa kuchagua kuwa kinara katika eneo hilo kwa kuwa eneo hilo ni muhimu katika kuendeleza jitihada za serikali katika kuleta usawa wa kijinsia.

mwakilishi wa UN WOMEN hapa nchini Hoden Haduu ameipongeza serikali ya Tanzania na kusema kuwa hatua hiyo itasaidia wanawake na wasicha kufurahia fursa sawa na kuweza kufikia malengo ya maendeleo endelevu .

katika kuhakikisha ahadi za nchi zinatekelezwa Rais Samia ameteua kamati ya kitaifa ya ushauri kuhusu kufanikisha utekelezaji ahadi za nchi iliyojumuisha wajumbe kutoka tanzania bara na visiwani inayoanza utekelezaji mwaka 2021-2026.