Dodoma FM

Wanawake wafurahishwa na utendaji kazi wa taasisi za kutetea haki za wanawake

14 December 2021, 12:31 pm

Na ;Thadei Tesha.

Wanawake waelezea jinsi wanavyo nufaika na taasisi mbalimbali zinazo tetea kundi la wanawake katika nyanja mbalimbali.

Taswira ya habari imefanya mahojiano na baadhi ya wanawake kuhusiana na Namna walivyonufaika na harakati mbalimbali zinazofanywa na mashirika dhidi yao.

Wamesema kuwa kwa sasa jamii kwa kiasi kikubwa imeanza kubadika kutoka kwenye Mfumo dume ambapo wamesema nguvu kubwa inahitajika zaidi Hasa kwa upande wa Vijijini ambapo mfumo dume bado upo hususani kwa wanawake wakulima.

Aidha wamezitaka taasisi mbalimbali zinazotoa elimu kuhusiana na suala hilo kuendelea na jitihada hizo ili kukuza uelewa zaidi kwa jamii juu ya athari za Mfumo dume .

Viongozi mbalimbali wamekuwa wakihamasisha kuhusiana na jamii kuacha kumkandamiza mwanamke ambapo afisa ustawi wa jamii wa Jiji la Dodoma amewashauri wanaume pamoja na wanawake kusimama katika jukumu lao ili kupinga ukatili dhidi ya wanawake kwani ofisi hiyo bado inapokea tarifa za ukatili.

Miongoni mwa mambo ambayo asasi mbalimbali pamoja na mashirika ya kuwatetea wanawake wamekuwa wakihamasisha ni suala la kumlinda mwanamke dhidi ya Mfumo dume ambapo baadhi ya jamii zimeanza kuelimika kuhusiana na suala hilo.