Dodoma FM

Kikosi cha usalama barabarani chaendeleza elimu juu ya matumizi sahihi ya barabara

14 December 2021, 11:51 am

Na; Yussuph Hans.

Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoani Dodoma kimesema kinaendelea kujikita zaidi katika kutoa elimu kwa watumiaji wa Barabara ili kujikinga na ajali za barabarani .

Akizungumza na kituo hiki Mkuu wa kikosi cha Usalama Barabarani SACP Boniface Mbao amesema kuwa utoaji wa elimu kuhusu usalama barabarani ni muhimu kwa watumiaji wa barabara, sambamba na hayo wamekuwa wakiendesha operesheni za kudhibiti mwendokasi.

Ameongeza kuwa wamekuwa wakifanya ukaguzi wa magari chakavu na kuwachukulia sheria watu wanaofanya makosa mbalimbali barabarani.

Taswira ya habari imezungumza na wakazi Mkoani Dodoma ambapo wametoa rai kwa watumiaji wa barabara kuzingatia sheria na alama za barabarani katika kipindi hiki cha kuelekea sikukuu za mwisho mwaka.

Ajali za barabarani zimekuwa tishio Nchini na Duniani kote licha ya jitihada mbalimbali zinazochukuliwa na Serikali kwa kushirikiana na wadau kuhakikisha ajali hizo zinakoma.