Dodoma FM

Wanaume watakiwa kuvunja ukimya dhidi ya vitendo vya ukatili

13 December 2021, 3:25 pm

Na; Thadei Tesha .

Kutohudumia familia kwa baadi ya wanaume kunapelekea wanaume hao kufanyiwa vitendo vya ukatili na wenza wao na kukaa kimya.

Taswira ya habari imefanya mahojiano na baadhi ya wananume kufahamu sababu zinazopelekea baadhi yao kusahau majukumu ya familia na kusababisha baadhi ya watoto kuharibikiwa kimaadili.

Wamesema miongoni mwa visababishi ni pamoja na baadhi ya wenza wao kuwa wakorofi jambo linalowafanya kujiingiza katika vitendo vya ulevi na kuwataka wanawake kuacha vitendo hivyo ikiwemo vipigo kwa waume zao.

kwa upande wake mkuu wa dawati la jinsia Wilaya ya Dodoma mjini Inspekta Jerda Luyangi amesema ofisi yake imeendelea kutoa elimu kwa jamiina kuchangia ongezeko la wanaume kuripoti vitendo vya ukatili dhidi ya wenza wao katika ofisi hiyo.

Aidha ametoa wito kwa serikali kuendelea kuunga mkono juhudi za mashirika mbalimbli ya kupambana na vitendo hivyo huku akisisitiza serikali kuwa mstari wa mbele kutatua changamoto mbalimbali zinazowakumba wao kama ofisi juu ya kupambana na vitendo vya ukatili.

Mara kadhaa viongozi na mashirika mbalimbali ya kifamilia wamekuwa wakisistiza jamii kuwa suala la malezi ni jukumu la kila mzazi ili kujenga watoto wenye maadili kwa ustawi wa jamii na taifa kwa ujumla.