Dodoma FM

Imeelezwa kuwa asilimia 70 watoto wenye ulemavu wa macho wamefaulu elemu ya msingi

10 December 2021, 12:25 pm

Na; Alfred Bulahya.

Imeelezwa kuwa asilimia 70 ya watoto wenye ulemavu wa macho waliosaidiwa kwa kupatiwa vifaa vya kusomea na kupewa kipaumbele shuleni, wamefaulu elimu ya msingi na kijiunga na sekondari.
 
Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa Shirika la Light For The World, Joseph Banzi, wakati akizungumza na waandishi wa habari, katika mkutano wa wadau mbalimbali wa kujadili namna watu wenye ulemavu wanapata fursa ya kuendelea na masomo bila ya kujali changamoto zao.
 
Amesema lengo la mkutano huo ni kubadilisha uzoefu kulingana na changamoto za watoto wenye ulemavu na namna kuwasaidia watoto hao huku akitaja aina ya changamoto zinazowakabili ni kukosa matibabu na kukosa vifaa vya kuwasaidia kupata elimu.
 

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Watu wenye Ulemavu (SHIVYAWATA), Ernest Kimanya, amesema wanaangalia njia bora zaidi ya kupata elimu jumuishi kwani tafiti zinaonyesha kuwa, changamoto bado zipo na zinafanya watoto wenye ulemavu kushindwa kupata elimu.