Dodoma FM

Jamii yatakiwa kuondoa hofu juu ya kuripoti matukio ya ukatili

8 December 2021, 2:20 pm

Na; Shani Nicolaus .

Wakati Tanzania ikiendelea kuungana na mataifa mengine katika kuadhimisha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia jamii imetakiwa kuondoa hofu juu ya kuripoti kesi za ukatili.

Akizungumza na Dodoma fm msimsamizi mkuu wa dawati la jinsia Mkoa wa Dodoma Inspekta Christer Kayombo amesema kila mtu anaeshiriki kutoa taarifa za matukio ya ukatili anatunziwa siri yake bila kuvujishwa mahali popote

Mkuu wa dawati la jinsi Wilaya ya Dodoma Inspekta Jelda Luyangi amesema kuwa elimu juu ya ukatili wa kijinsia Nchini bado haija jitosheleza hivyo kuna haja ya kuwa na elimu endelevu katika sehemu tofauti pamoja na utoaji haki pale hukumu zinapotolewa.

Amesema kuwa chanzo kikubwa cha ukatili kinachangiwa na sababu mbalimbali ikiwemo mila na desturi potofu ambazo zinachangia kwa kiasi kikubwa kuchochea ukatili wa kijinsia Nchini.

Baadhi ya wananchi jijini hapa wamesema kilio chao ni juu ya Serikali kuiomba kukomesha ukatili hasa kwa kutoa adhabu kali kwa wahusika pamoja na kuweka sheria kali kwa yeyote atakaehusika kukwamisha kesi hizo.

Siku kumi na sita za kupinga ukatili zinaendele kuadhimishwa ulimwenguni ambapo kila Mtanzania ana husika kwa kushiriki kutoa taarifa za matukio ya ukatili ambapo maadhimisho hayo yamebebwa na kaulimbiu isemayo “Ewe Mwananchi Pinga Ukatili Dhidi Ya Mwanamke”